Serikali ya kaunti ya Nyamira imetenga shillingi millioni 30 kufanya miradi ya maendeleo.
Miongoni mwa maendeleo ambayo yanatarajiwa kufanywa katika wadi zote 20 za kaunti hiyo ni kufungua barabara, kuchimba vizima vya maji, kuboresha hospitali ili kutoa huduma bora za matibabu ya kiwango kinachostahili , kuboresha vyuo vya kiufundi miongoni mwa mengine .
Akizungumza siku ya Alhamisi mjini Nyamira, gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama alisema serikali yake imeimarisha mikakati ya kuhakisha maendeleo yamefanywa kiukamilifu katika kaunti yake
“Serikali yangu imetenga pesa ili kufanya maendeleo katika sehemu mbalimbali za kaunti na vijana 20 wataajiriwa kwa kila wadi kufanya miradi hiyo ya maendeleo,”alisema gavana Nyagarama.