Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya kaunti ya Nyamira imetenga shillingi millioni tano kukarabati soko la Nyabite lililoko eneo bunge la Mugirango Magharibi.

Hii ni Baada ya wafanyibiashara wa soko hilo kuhimiza serikali hiyo kuharakisha ujenzi wa soko hilo ili kuwaruhusu kurejelea shughuli zao za kibiashaara kama kawaida.

Akizungumza nasi siku ya Alhamisi mjini Nyamira waziri wa Biashara katika kaunti hiyo, John Omanga alisema serikali hiyo imetenga pesa hizo ili kuhakikisha ujenzi wa soko hilo umekamilika hivi karibuni.

“Sisi kama serikali tutajaribu kuhakikisha ukarabati wa soko la Nyabite umekamilika kwa muda unaofaa maana tayari tumetenga shillingi millioni tano za kushughulikia ujenzi huo,” alisema  Omanga.

Aidha, Omanga alisema serikali ya Nyamira iko katika mstari wa mbele kuhakikisha sekta ya biashara imeshughulikiwa vilivyo ili kuinua uchumi wa kaunti hiyo na katika taifa la Kenya kwa ujumla.

Omanga aliomba wafanyibiashara kufanya biashara zao kwa bidii ili kuhakimkisha kaunti ya Nyamira imeinuka kiuchumi.

Pia aliongeza kusema serikali iko tayari kutoa usaidizi kwao kujiendeleza kupitia biashara na maendeleo mengine mengi.