Serikali imetakiwa kuliondoa jeshi lake nchini Somalia, ili kumaliza mashambulizi yanayotokea nchini na kutatiza sekta ya utalii.
Akizungumza katika eneo la Malindi siku ya Jumanne, Seneta wa Kakamega Bonny Khalwale, alisema kudorora kwa sekta ya utalii kumechangiwa na ukosefu wa usalama nchini.
Khalwale alisema kuwa serikali sharti iondoe jeshi la KDF kutoka Somalia, na kuliweka mpakani mwa taifa ili kuliwezesha kupambana na magaidi.
Seneta huyo alisisitiza kuwa kuondolewa kwa jeshi hilo nchini Somalia kutamaliza mashambulizi yanayotekelezwa humu nchini na wafuasi wa al-Shabaab, sawia na kukomesha maafa yanayowakumba wanajeshi wa Kenya.