Kijana mmoja alifikishwa mahakamani siku ya Jumatatu kwa tuhuma za kupatikana na bangi.
Upande wa mashtaka ulielezea mahakama kuwa mnamo Novemba 28, 2015, mshukiwa, Ahmed Mohamed Ahmed, alipatikana na misokoto mitatu ya bangi katika eneo la Ganjoni.
Hata hivyo, Ahmed alikanusha madai hayo mbele ya Hakimu Diana Mochache.
Ahmed aliambia mahakama kuwa yeye ni mtumizi wa dawa ya Methadone wala sio bangi, na polisi walimikamata kwa kudhania yeye ni mtumizi wa mihadarati.
“Mimi ni kati ya watumizi wanaotumia dawa ya Methadone ili kuniwezesha kuacha utumizi wa mihadharati. Polisi walininasa kimakosa nilipokuwa katika bishara yangu ya kuuza nguo,” alisema Ahmed.
Hakimu Mochache alimwachilia kwa dhamana ya shilingi 100,000.
Kesi hiyo itasikilizwa Aprili 14, 2015.