Share news tips with us here at Hivisasa

Bunge la kaunti ya Mombasa siku ya Jumatano liliidhinisha hoja ya kubuni kituo maalum cha kuhudumia watoto wanaodhulumiwa kingono.

Hoja hiyo iliyowasilishwa bungeni na mwakilishi mteule Mary Akinyi inasema visa vya watoto kudhulumiwa kingono vimeongezeka na kituo hicho kitasaidia kukabili tatizo hilo.

“Hapo awali kulikuwa na kituo ambacho kilikuwa kinaendeshwa na serikali kuu ambapo walikuwa wameweka nambari ya simu ya 116  lakini ilikuwa ukipiga haifanyi kazi.

Sasa ndio maana nikaja na hili wazo la kuwa na kituo maalum hapa Mombasa,” Akinyi alisema.

Kituo hicho kitakuwa na nambari ambazo wale wenye taarifa za watoto kudhulumiwa watapiga ripoti, na kitakuwa chini ya idara ya polisi.