Machifu wote katika eneo bunge la Borabu kaunti ya Nyamira wameombwa kuhakikisha kila mwanafunzi ambaye alituma ombi la kufadhiliwa kwa pesa za 'basari' amefadhiliwa.
Akizungumza siku ya Jumatatu katika eneo bunge lake Mbunge wa eneo hilo Ben Momanyi alisema kila mwanafunzi yeyote aliyejaza fomu ya ufadhili ya pesa za 'basari' kupitia Hazina ya Ustawi wa Maeneo Bunge (CDF) amepewe pesa hizo ili kuendeleza masomo.
Momanyi pia aliwaomba machifu kuhakikisha pesa ambazo hutumwa kwa njia ya 'Cheque' hazipotei.
Momanyi alitoa shillingi millioni 10 kutoka kwa hazina ya CDF kufadhili masomo kwa wanafunzi ili waendeleza masomo.
“Naomba machifu kujaribu kila wawezalo kuhakikisha kila mwanafunzi aliyetuma ombi la 'basari' amepokezwa pesa za ufadhili ili aendeleza elimu,” alisema Momanyi.
Momanyi aliomba wanafunzi wote katika eneo bunge lake la Borabu kutia motisha kwa masomo ili kupita katika mithani ya kitaifa
“Ikiwa mwanafunzi anahitaji maisha mema katika siku sijazo sharti awe na motisha kwa kusoma naomba kila mwanafunzi kusoma kwa bidii,” aliongeza Momanyi.