Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Afisa mkuu wa kitengo cha trafiki wilayani Kisii ya kati Erick Gitinji amepiga marufuku magari aina ya 'probox' kutumika kusafirisha abiria .

Kulingana na afisa huyo, magari hayo hayakubaliwi kutumika barabarani kama matatu, huku akisema yeyote atakayefumaniwa atatiwa mbaroni kwani ni kinyume na sheria kutumia magari hayo.

Akizungumza siku ya Jumanne mjini Kisii, Gitinji alisema magari hayo yamekuwa yakihusika katika visa vya ajali barabarani kila wakati na kujeruhi wengi, huku akisema magari hayo yaondolewe barabarani.

“Magari aina ya probox yameongezeka barabarani kufanya uchukuzi, naomba magari hayo yaondolewe na yafanye kazi nyingine tofauti kando na kusafirisha abiria,” alisema Gitinji, afisa mkuu wa trafiki wilayani Kisii ya kati.

“Ni ukiukaji wa sheria za barabarani wakati magari hayo yanafanya uchukuzi, yeyeote atakayepatikana kutumia magari hayo kwa sekta ya uchukuzi basi atakabiliwa na sheria kali baada ya kutiwa mbaroni,” aliongeza Gitinji.

Hapo mapema, wakazi wa kaunti ya Kisii waliomba magari hayo kupigwa marufuku kwa kile walichokisema kuwa husika katika visa vya ajali kila wakati jambo ambalo limepata mhamko na afueni kwa wakazi kwani walipendekeza hilo kufanyika.