Share news tips with us here at Hivisasa

Mwenyekiti wa chama cha wanasheria kwenye kanda ya mkoa wa bonde la ufa wakili David Mong’eri amesema majaji wanafaa kustaafu wakiwa na umri wa miaka 70.

Mwenyekiti huyo alisema ingawa katiba ya zamani imeweka bayana kuwa majaji wanafaa kustaafu wakiwa na umri wa miaka 74, wanafaa kubaini kwamba katiba ya sasa inayosema majaji wanafaa kustaafu wanapofikisha umri wa miaka 70 ndiyo inayotumika.

Matamshi yake yanajiri baada ya ombi la naibu jaji mkuu Kalpana Rawal la kutaka kustaafu katika umri wa miaka 74 kutupiliwa mbali na mahakama ya juu.

Hata hivyo, mahakama ya rufaa ilimruhusu naibu wa jaji mkuu kalpana rawal kukata rufaa dhidi ya kesi iliyowasilishwa mahakamani na tume ya huduma za mahakama jsc ya kumtaka astaafu baada ya kutimiza umri wa miaka 70.