Share news tips with us here at Hivisasa

Mama mmoja pamoja na watoto wake watatu wamejeruhiwa vibaya  baada ya kuhusika kwenye ajali mbaya kwenye barabara ya  kivuko cha Likoni kuelekea Ukunda.

Ajali hiyo ilihusisha tuk tuk mbili zinazodaiwa zilikuwa zinaendeshwa kwa kasi.

Kulingana na Sam Muya ambaye alishuhudia ajali hiyo siku ya Jumapili usiku, alisema kuwa  tuk tuk hizo ziligongana baada ya moja kupoteza mwelekeo.

“Nadhani dereva mmoja alikosa kuona vizuri ndio ikasababisha ajali hii,” alisema Muya.

Madereva hao walichukuliwa na polisi wa kituo cha polisi cha Likoni huku waliojeruhiwa wakipelekwa katika hospitali ya Likoni Level 4.