Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kufuatia hali ya watoto wasichana kukosa kuhudhuria shule kwa siku kadhaa kwasababu yakukosa visodo.

Mwakilishi wa kina mama katika kaunti ya Nyamira Alice Chae amejitokeza kuyataka mashirika yasiyokuwa yakiserikali kujitokeza kusaidia kupunguza visa hivyo. 

Akihutubia wanahabari mjini Nyamira, Chae alisema kuwa yafaa mashirika yasiyokuwa yakiserikali kujitokeza ili kusaidia katika ununuzi wa visodo ili kuwawezesha wasichana kuhudhuria shule. 

"Wakati umefika ambapo sasa yafaa mashirika yasiyokuwa yakiserikali kujitokeza kununua visodo ili kuvisambaza katika shule mbalimbali ili kuwawezesha wasichana wanaoathirika na hali yakukosa visodo kuhudhuria shule," alisema Chae. 

Chae aidha, aliongeza kwa kusema kuwa wasichana wengi wanaotoka katika familia maskini hukosa kuhudhuria shule kutokana na hali yakukosa visodo hali aliyosema huathiri pakubwa masomo yao huku akihoji kuwa hali hiyo inafaa kushughulikiwa. 

"Masomo ya wasichana wengi hasa wale walio katika shule za msingi huathirika zaidi kutokana na hali yakukosa visodo wakati wa hedhi," alisema Chae.

"Na kwa hakika serikali yakitaifa yahitajika kushughulikia hali hii ili kuhakikisha kuwa wasichana wanahudhuria shule bila ya matatizo," aliongeza Chae.