Hatma ya mwakilishi mmoja mteule kutoka jimbo la Nakuru haijulikani baada ya kudaiwa kukosa kulipa deni la shilingi 200,000, hela za mfanyibiasara mmoja mjini humo.
Kulingana na mfanyibiashara Francis Gitau ni kuwa mwakilishi huyo amedinda kulipa hela hizo hata baada ya jitihada zake za mara kwa mara za kudai.
Kulingana na Gitau ni kuwa alimpa Margaret Wanjiku Kiiru hela hizo mnamo Januari 26 2016 alizodai analipa deni la benki na kisha arejeshe ili mfanyibiashara huyo aweze kundeleza biashara zake, ahadi ambazo hadi sasa zimegonga mwamba.
“Nilimpa pesa hizo kwa sababu alikuwa anasema alitaka kulipa deni la benki, na kama mhisani na mtu ninayemheshimu, nilimpa hela hizo na akaahidi kurudisha lakini hadi kufikia hadi sasa sijalipwa,” Gitau alisema.
Akiongea Al hamisi, MCA huyo alikiri kupata mkopo huo lakini akasema amechelewa kulipa.