Mwakilishi wadi ya Elburgon Florence Wambui amewataka vijana kujiepusha na siasa potovu.
Akizungumza Jumamosi katika soko la Elburgon,Wambui alisema kuwa vijana ni nguzo muhimu lakini huenda wakapotoshwa na baadhi ya wanasiasa.
"Vijana ni nguzo muhimu kuwa taifa lakini ili kufaulu,wanafaa kuepuka siasa potovu,"Wambui alisema.
Mwakilishi huyo wa wadi vilevile aliwasuta wanasiasa wanaoendeleza ukabila katika kaunti ya Nakuru.
Kwa mujibu wake,viongozi wanafaa kuendeleza siasa komavu za kuwaunganisha wakaazi wote wa Nakuru.