Mkuu wa polisi kaunti ya Mombasa Martin Asin amefariki baada ya kuhusika katika ajali mbaya ya barabarani eneo la Maungu barabara kuu ya Mombasa kuelekea Nairobi.
Akithibitisha kisa hicho, mshirikishi wa serikali kanda ya pwani Nelson Marwa amesema kuwa Asin amekumbana na kifo chake alipokua anaelekea jijini Nairobi.
Kifo chake ni pigo kubwa kwa waandishi wa habari ambao wamekuwa wakishirikiana naye kuhusiana na mambo ya usalama katika kaunti ya Mombasa.
Bwana Yasin amekua na usaidizi mkubwa haswa katika mchango wake wa kuhakikisha kuwa kaunti ya Mombasa inasalia kuwa salama.
Marwa aidha amesema uchunguzi unaendelea kubaini zaidi kuhusiana na ajali hiyo.
Mwendazake mkuu wa polisi kaunti ya Mombasa Martin Asin. Aliaga dunia baada ya kuhusika katika ajali mbaya ya barabarani hii leo, Jumanne.