Share news tips with us here at Hivisasa

Kesi moja ya wizi wa mabavu imeondolewa kwenye mahakama ya Winam jijini Kisumu baada ya mlalamishi kuamua kumsamehe mshtakiwa.

Gordon Ochieng ameondoa kesi hiyo mahakamani, baada ya mshtakiwa ambaye ni nduguye kwa jina Charles Otieno kumwomba msamaha.

Mahakama ilikuwa imeambiwa kuwa mnamo tarehe 5 mwezi Novemba mwaka huu katika kijiji cha Kolwa, kaunti ya Kisumu, Charles Otieno, ambaye alikuwa amejihami kwa kisu alimvamia nduguye na kumnyang’anya simu moja ya rununu aina ya tecno, kitambulisho cha kitaifa na shilingi 2,500 pesa taslimu; vyote vyenye thamani ya shilingi 5,000.

Mshtakiwa alikuwa amekanusha shtaka na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki mbili alipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mnamo tarehe 17 mwezi jana.

Kesi hiyo ilifaa kuendelea kusikilizwa tarehe 21 mwezi wa Aprili mwaka ujao, lakini hakimu Banard Kasavuli wa mahakama ya Winam hawakua na lingine ila kuitupilia mbali, baada ya mlalamishi kuamua kumsamehe kakake.