Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamke mwenye umri wa makamo amefikishwa katika mahakama ya Mombasa kwa tuhuma za mauaji bila kukusudia.

Upande wa mashtaka ulielezea mahakama siku ya Jumatatu kuwa mnamo Novemba 9, 2015, mshukiwa, Mary Adhiambo, anadaiwa kumdunga kisu Ali Juma, baada ya kutofautiana kuhusu bei ya chang’aa katika eneo la Namba Tano huko Likoni.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikana mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkuu Susan Shitub.

Hakimu Shitub alimtoza Adhiambo dhamana ya Sh500,000 na mdhamini wa kiasi sawa.

Kesi hiyo itasikilizwa Februari 2, 2016.