Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamume mmoja alifikishwa mahakamani kwa kosa la kumnajisi msichana wa miaka 15.

Mshukiwa huyo, Collins Kavanze, aliyefikishwa mbele ya mahakama moja ya Nakuru siku ya Jumatano anadaiwa kutekeleza kosa hilo tarehe Julai 10, 2015 katika Mtaa wa Flamingo, ulio viungani mwa mji wa Nakuru.

Mshtakiwa huyo alikana kosa hilo mbele ya Hakimu Mkuu wa Nakuru Liz Gicheha.

Kavanze aliachilia kwa bondi ya Sh200,000.

Kesi hiyo itatajwa Novemba 12, 2015 na kusikizwa Januari 21, 2016.