Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamke mmoja anayekabiliwa na mashtaka mawili moja likiwa kupatikana na stakabadhi bandia atalazimika kusalia rumande hadi mwaka ujao iwapo atakosa dhamana ya Sh100,000.

Mshtakiwa, Susan Mwangi, anadaiwa kupatikana katika benki ya Kenya Women Finance Trust (KWFT) tawi la Nakuru, akijaribu kutoa pesa kutoka kwa akaunti ya Pauline Kigera mnamo Oktoba 22, 2015.

Upande wa mashtaka ulidai kwamba mshtakiwa alipatikana na kitambulisho bandia kilichokuwa na jina la Grace Pauline Wanja Kigera.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikana mashtaka hayo siku ya Jumatatu mbele ya Hakimu mkuu wa Nakuru Doreen Mulekyo.

Mwangi aliachiliwa kwa bondi ya Sh100,000 au Sh60,000 pesa taslimu.

Kesi hiyo itatajwa Novemba 16, 2015 na kuskizwa Januari 29, 2016.