Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamume mmoja amefikishwa mahakamani kujibu shtaka ka kupatikana akiuza dawa za kulevya.

Upande wa mashtaka ulielezea mahakama siku ya Juamatatu kuwa mshukiwa, Benard Ramogi, anadaiwa kupatikana akiuza pakiti 22 za heroine, zenye thamani ya shilingi 4,400, mnamo Januari 9, 2016 katika eneo la Sega Majengo, Kaunti ya Mombasa.

Mshukiwa huyo alikana madai hayo mbele ya Hakimu katika Mahakama ya Mombasa Richard Odenyo.

Hakimu Odenyo alimpa Ramogi dhamana ya shilingi 100,000.

Kesi hiyo itasikizwa mnamo Januari 27, 2016.