Share news tips with us here at Hivisasa

Mwakilishi wa Wadi ya Sensi Onchong’a Nyagaka amefadhili masomo ya wanafunzi 41 ambao wanatarajia kujiunga na kidato cha kwanza.

Wanafunzi hao ambao walipata alama zaidi ya 300 katika mtihani wa kitaifa wa KCPE mwaka jana, pia walipokezwa godoro na sanduku ya vitabu kila mmoja.

Akizungumza siku ya Jumatatu katika eneo la Sombogo alipokuwa anatoa ufadhili huo, Nyagaka alisema hiyo ni njia mojawapo ya kuwapungunzia wazazi mzigo wanapowapeleka wanao shuleni.

Nyagaka alitimiza ahadi yake baada ya kuahidi kutoa ufadhili huo haswa kwa wanafunzi ambao watapata alama hizo, kabla ya mtihani huo kuanza mwaka jana.

“Mimi kama mwakilishi wa wadi nitaendelea kutoa ufadhili wa aina hii. Mwaka ujao nitatoa ufadhili huu ili wazazi wasiwe wanapata changamoto mnapowapeleka watoto wenu shuleni,” alisema Nyagaka.

Aliongeza, “Kila mzazi anapaswa kuhakikisha masomo yanapewa kipau mbele ili kuleta usaidizi katika jamii yetu. Pia ningependa kuwaomba kushirikiana nami katika uongozi huu ili kuleta maendeleo.”

Aidha, Nyagaka aliomba kila mkaazi kuchukua kitambulisho na kujiandikisha kama mpiga kura ili kuchagua viongozi watakao leta maendeleo katika taifa la Kenya.