Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakaazi wa wadi ya Mekenene wamepata sababu ya kutabasamu baada ya mwakilishi Alfayo Ngeresa kuanzisha mradi wa kujenga kituo cha masomo.

Akihutubu alipotembelea mradi huo siku ya Jumanne, Ngeresa alisema kuwa kituo hicho kitawasaidia pakubwa wanafunzi kutoka eneo hilo kupata vifaa, hasaa vitabu vya marejeleo, vitakavyo wawezesha kusoma.

Ngeresa alisema kuwa kituo hicho kitasimamiwa na wataalamu pindi ujenzi utakapo kamilika.

"Kwa kweli shule zetu za umma zimekuwa zikifanya vibaya kwenye mitihani ya kitaifa. Hatahivyo, kupitia kwa mradi huu unaofadhiliwa na wakfu wangu, kituo hicho cha masomo kitakacho gharimu zaidi ya shillingi millioni 15 kitajengwa,” alisema Ngeresa.

Ngeresa aidha alisema kuwa kituo hicho kitakacho wahifadhi zaidi ya wanafunzi 200 kitafunguliwa siku zote za juma ili kuwasaidia wanafunzi kupata nafasi za kufanya marudio yao ya darasani.

"Kituo ambacho tunakijenga kitakuwa wazi kwa siku saba za wiki ili kiwasaidie wanafunzi na hata pia wakaazi wote wa eneo hili kupata nafasi ya kusoma," alisema Ngeresa.

Ngeresa vilevile alishukuru shirika la Sir John Leeman kutoka uingereza kwa kufadhili mradi huo na hata pia kwa kununua vitabu vitakavyo wasaidia wanafunzi kufanya marejeo yao ya darasani.

"Kwa niaba ya wakfu wa Ngeresa ningependa kushukru shirika la John Leeman kwa kujitolea kwake kufadhili mradi huu muhimu, kwa kuwa utawasaidia pakubwa watoto wetu," alisema Ngeresa.