Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kufuatia ongezeko la ajali kwenye barabara ya Nakuru-Nyahururu, mwanaharakati David Kuria ametoa wito kwa mamlaka ya uchukuzi na usalama barabarani, NTSA, kuimarisha vita dhidi ya madereva wasiotii sheria. 

Mkurugenzi huyo wa shirika la Nakuru Human Rights Network alisema kuwa iwapo NTSA haitakaza kamba, vifo vitaendelea kushuhudiwa barabarani.

"Litakuwa jambo la busara iwapo mamlaka ya NTSA itawajibika zaidi kurejesha nidhamu barabarani,"alisema Kuria.

Wakati huo huo,mwanaharakati huyo ametoa wito kwa wakaazi wa kushirikiana na idara ya usalama Nakuru katika kumaliza wahalifu. 

Alikuwa akizungumza wakati wa kikao na wanahabari katika eneo la White House, Nakuru.