Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwanamke mmoja alifikishwa kwenye mahakama moja ya Nakuru siku ya Jumanne kujibu shtaka la kusababisha kifo cha mtoto wake kwa kumtupa chooni.

Mshtakiwa, Ivy Chelagat, anadaiwa kwamba alikusudia kusababisha kifo cha mtoto wake kwa kumtupa katika choo mnamo Desemba 22, 2015 katika zahanati ya Tuiyotich, kwenye kaunti ndogo ya Njoro.

Mahakama ilielezwa kuwa mtoto huyo alikuwa amezaliwa siku saba kabla ya tukio hilo, na alikuwa angali hospitalini akisubiri kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Hata hivyo, Chelagat alikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkuu Maroro Nyakundi, na kuachiliwa kwa bondi ya Sh100,000 na mdhamini wa kiasi sawia au Sh 50,000 pesa taslimu.

Kesi hiyo itasikizwa Februari 16, 2016.