Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamke mmoja pamoja na mwanawe walifikishwa mahakamani kwa kosa la kuuza pombe haramu.

Margaret Wangila na Emmanuel Juma walipatikana na lita 80 za chang’aa katika eneo la Tudor.

Wawili hao walikubali mashtaka hayo mbele ya Hakimu mkuu wa Mombasa Susan Shitub siku ya Jumatatu.

Margaret aliambia mahakama kuwa hali ya umasikini na jukumu la kulipa karo za wanawe 10 ndilo lilompelekea kuendeleza biashara hiyo ya chang’aa.

Wangila aliomba mahakama kumsamehe na kumuachilia kwa faini ya kiasi kidogo na kuahidi kutofanya biashara hiyo tena.

Hakimu Shitub alikubali ombi hilo na kuwatoza faini ya Sh15,000 ama kutumikia kifungo cha miezi mitatu gerezani.

Washitakiwa hao wana siku 14 za kukata rufaa kupinga uamuzi huo.