Mwanamume mmoja amefungwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani kwa kosa la kuiba bidhaa za nyumbani.
Mahakama ilielezwa kuwa mshukiwa, Sylvester Kilonzo, aliiba mali ya thamani ya shilingi elfu 14 katika Soko la Mwembe Tayari mjini Mombasa, mnamo Disemba 13, 2015.
Mali hiyo ilijuimisha leso 25 zenye thamani ya shilingi elfu 2,500, kilo moja ya maziwa ya unga, mifuko sita ya unga wa ngano, kilo mbili za sukari na mafuta ya kupikia, zote mali ya Rose Kalondu Moses.
Kilonzo alikubali madai hayo siku ya Jumatano katika mahakama ya Mombasa mbele ya Hakimu Diana Mochache.
Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mochache alisema kuwa hukumu hiyo itakuwa funzo kwa wengine wanaojihusisha na wizi.