Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamume wa umri wa miaka 42 John Mwanzo, amehukumiwa kifo kwa kwa kosa la ubakaji na mauaji ya mtoto wa miaka tano.

Akitoa hukumu hiyo siku ya Jumatatu, Jaji Martin Muya alisema kuwa kulingana na ushahidi uliotolewa, ni wazi kuwa mshtakiwa alihusika katika mauaji hayo, ikizingatiwa kulipatikana damu juu ya godoro la mshukiwa huyo.

Aliongeza kuwa marehemu alipatikana akiwa amefariki ndani ya chumba cha mshukiwa huyo huko Kizingo.

Aidha, aliongeza kuwa uchunguzi wa vinasaba vya DNA ulionyesha kuwa mshukiwa huyo ndiye aliyehusika katika ubakaji wa mtoto huyo ikizingatiwa alimuharibu sehemu zake za siri wakati wa kitendo hicho.

Mshukiwa huyo ana siku 14 za kukata rufaa kupinga kifungo hicho.

Wiki iliyopita, jaji Martin Muya alimpata mshukiwa huyo na hatia ya mauaji na ubakaji ya mtoto huyo.

Mshtakiwa John Mwanzo anadaiwa kumbaka hadi kufariki mtoto huyo wa miaka mitano katika eneo la Kizingo mnamo Disemba 30, 2012.