Mwanamume wa umri wa makamo amefungwa miaka saba gerezani kwa kosa la mauaji bila kukusudia.
Mshtakiwa, Mourice Wepekhulu, anadaiwa kumua Kassim Balimo Adoli katika eneo la Bangladesh huko Changamwe, mnamo Julai 13, 2013.
Akitoa hukumu hiyo siku ya Ijumaa, Hakimu Martin Muya, alisema kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa, ni dhahiri kuwa mshukiwa alimuua marehrmu pasi kukusudia.
Mshtakiwa huyo alipewa siku 14 za kukata rufaa kupinga kifungo hicho.