Mwanamume wa makamo ametozwa faini ya shilingi elfu kumi au kifungo cha miezi sita gerezani baada ya kupatikana na dawa za kulevya.
Upande wa mashtaka ulieleza mahakama kuwa mshtakiwa, Said Chikobe, alipatikana na misokoto 42 ya bangi yenye thamani ya shilingi 840, mnamo Desemba 17, 2015 katika eneo la Tudor Moroto.
Mahakama ilithibitisha kuwa misokoto hiyo ilikuwa ya dawa za kulevya aina ya bangi kulingana na uchunguzi uliofanywa katika maabara ya serikali.
Chikobe alikubali madai hayo siku ya Jumatano, mbele ya Hakimu Richard Odenyo.