Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanaume mmoja anayeshukiwa kuwa mchawi alichomwa moto usiku wa kuamkia Alhamisi na umati wa watu uliyokuwa umejawa na ghadhabu katika kijiji cha Giachong’e eneo bunge la Bahati.

Akidhibitisha kisa hicho chifu wa Dundori Muthoni Mutuku alisema kuwa marehemeu kwa jina la Shadrack Karuma Kiboi, aliuawa baada ya kudaiwa kuwa chanzo cha kifo kisichokuwa cha kawaida cha dadake Phoebe Njoki mwenye umri wa miaka 58, baada ya kupata matatizo ya tumbo na kupelekea tumbo lake kufura.

Aidha chifu huyo ameongeza kuwa siku mbili zilizopita alimwokoa marehemu baada ya umati huo kutaka kumteketeza.

Vilevile kwa mujibu wa wakaazi wa eneo hilo wanadai kwamba kuku wa marehemu kiboi walikufa siku tatu zilizopita na kutoa vitisho kwa dada yake ya kwamba atafariki siku tatu baada ya kuku huyo kuanza kuoza, jambo ambalo wanadai lilitokea.

Marehemu aidha anasemekana kuwa ndugu ya mmoja wa wazee wa mtaa katika kijiji hicho huku akiulizwa kusawazisha madai dhidi yake katika kijiji chicho.

Hata hivyo chifu huyo ametoa wito kwa wakaazi hao kutochukua sheria mikononi mwao na badala yake wafuate sheria ili hatua muafaka zichukuliwe dhidi ya watuhumiwa.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika ufuo wa kaunti ya Nakuru.