Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwenyekiti wa mamlaka ya usafiri na usalama barabarani hapa nchini, NTSA Lee Kinyanjui ametangaza rasmi kuwania wadhifa wa ugavana katika kaunti ya Nakuru.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa atakuwa katika kinyang’anyiro cha uongozi wa kaunti atakapokamilisha muda wake kama mwenyekiti wa NTSA Septemba mwaka huu.

Mwenyekiti huyo alikuwa mbioni katika uchaguzi mkuu uliopita na gavana wa sasa wa kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua, lakini akaangushwa katika mchujo na akajiunga katika timu ya kampeni ya rais katika uchaguzi uliopita.

Lee kinyanjui ni mmoja wa viongozi ambao wameonyesha azma yao ya kuwania wadhifa wa ugavana baada ya mweneykiti wa NACADA John Mututho kuonyesha azma sawa.

Aliyasema hayo siku ya Jumamosi iliopita alipojumuika katika hafla ya kuchangisha pesa za kugaramia malipo ya hospitali ya mwenyekiti wa maendeleo ya wanawake kaunti ya Nakuru Keziah Ngenah, katika hoteli moja mjini Nakuru.