Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwili wa mwanamke mmoja wa umri wa makamu Esther Wanza umepatikana nyumbani kwake katika eneo la Tala katika kaunti ndogo ya Matungulu ukiendelea kuoza siku ya Ijumaa.

Akidhibitisha kisa hiki, naibu was chifu wa Tala Francis Mulinge alisema kuwa mwanamke huyo mfanyabiashara katika soko la Tala na chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana.

Aidha Mulinge alisema kuwa polisi wameanzisha uchunguzi ili kubaini kilichomuua mwanamke huyo.

"Mwanamke huyo amepatikana amekufia kwake lakini bado chanzo cha kifo chake hakijabainishwa," alisema Bw Mulinge.

Vilevile, Mulinge aliwaomba wenyeji was Soko hilo kupeana habari zinazoweza kusaidia kubaini chanzo cha kifo cha marehemu.

Baadhi ya wafanya biashara katika Soko laTala waliokuwa wakifanya kazi na mwanamke huyo walielezea kuwa mwanamke huyo alikuwa akiishi peke yake na imekuwa muda wa siku tano alipoonekana sokoni humo.

"Imekuwa muda kabla tumuone sokoni na tumekuwa tukishangaa yupo wapi hadi pale maiti yake imepatikana kwake," alisema Ann Katile mwenyekiti was Soko la Tala.

Mwili was mwanamke huyo ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Kangundo Level Four.