Share news tips with us here at Hivisasa

Naibu gavana wa county ya Uasin Gishu Daniel Chemno ametoa wito kwa vijana kujitokeza kwa wingi ili kujiandikisha kama wapiga kura.

Akizungumza afisini mwake siku ya Jumanne, Chemno alisema kuwa vijana wajisalili ili wapate nafasi ya kuchagua kiongozi wanayempenda.

"Ni haki kisheria kila Mwananchi kumchagua anayempenda na tunaweza afikia malengo yetu ikiwa tuliowachagua watatuwakilisha vyema, hii inawezekana kwa kujisajili kwanza kama mpiga kura," alisema Chemno. 

Naibu gavana huyo aliwasihi wale ambao hawajachukua vitamblisho vyao kwenye afisi za kamishna kuvichukua ili waweze kujisajili. 

"Tumepata habari kwamba kuna vitambulisho ambavyo bado havijachukuliwa katika afisi ya usajili, nawahimiza tafadhali mvichukue," alisema chemno.