Shirika la ndege nchini la Kenya Airways limeelekeza ndege tatu zilizotarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKIA Nairobi kuja Mombasa na Kilimanjaro Tanzania kwa muda kutokana na hali mbaya ya hewa.
Maafisa wa shirika hilo kupitia akaunti yao ya twitter walithibitisha kuwa Ndege hizo aina ya KQ765, KQ499 na KQ552 zilizotarajiwa kutua saa 12 asubuhi, zilielekezwa Mombasa na Kilimanjaro Tanzania kutokana na hali tata ya anga asubuhi ya leo jijini Nairobi.
Hata hivyo, muda wa kutua kwa ndege hizo uliratibiwa upya, na zilitarajiwa kung’oa nanga Mombasa kurudi Nairobi.
Ndege aina ya KQ765 ilitarajiwa kuwasili Nairobi saa 3:15 asubuhi, ile aina ya KQ499 ikitarajiwa kuwasili saa 3:17 asubuhi ilhali ile aina ya KQ552 ikatarajiwa kutua saa 3:46.