Gavana wa Mombasa Hassan Joho amesema ODM haitaunga mkono mrengo wa Jubilee katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2017.
Akizungumza katika eneo la Malindi siku ya Jumatatu, Joho alisema kuwa ODM itapeperusha bendera ya uraisi kupitia mrengo wa Cord wala hawana nia yoyote kushawishiwa kisiasa kuunga mkono mirengo yoyote.
Aliongeza kuwa Cord iko imara na imejipanga kikamilifu kuwania kiti cha urais, na kuongeza kuwa wanaimani watashinda kiti hicho katika uchaguzi wa mwaka ujao.
Aidha, aliwataka wapiga kura kuhakikisha wanapigia kura viongozi wa Cord ili mabadiliko ya uongozi yapatikane kwa haraka nchini.
Kauli yake inajiri baada ya kushudiwa baadhi ya wanachama wa Cord kuuhama mrengo huo na kujiunga na Jubilee.