Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Hatua ya hivi karibuni ya muungano wa Cord kuwatimua wanachama waasi imeendelea kuzua hoja na kutetewa na wanachama waaminifu wa muungano huo.

Seneta wa Kaunti ya Mombasa Hassan Omar, amejitokeza na kutetea hatua ya hivi majuzi ya kuwatimua wanachama waasi na nafasi zao kuzibwa na wanachama wengine.

Omar alisema kuwa hatua ya kutimuliwa kwa mbunge wa Lunga Lunga Hatib Mwashetani, kutoka katika kamati ya bunge, ilikuwa na mtazamo wa kudhibiti na kuzuia uasi zaidi miongoni wa wale wanao nia mbaya dhidi ya chama hicho.

Seneta huyo ambaye alikuwa akiongea jijini Mombasa siku ya Jumamosi, alisema kuwa Cord kama muungano ambao una zaidi ya vyama vitano kwa pamoja, utaendelea kuwapa imani wafuasi wa muungano huo sababu wanataka kupata ushindi ifikapo uchaguzi mkuu ujao.

Kwa upande wake, Seneta Bonny Khalwale ambaye waliandamana na Omar aliwataka wafuasi wa muungano huo kuwa na imani wanapoendelea kupigania haki za kila Mkenya ambaye amedhulumiwa kwa njia moja au nyingine na serikali ilioko mamlakani.