Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Polisi eneo la Kithimani wamemtia mbaroni mwanamume mmoja anayedaiwa kujaribu kuiba pesa kutoka duka moja la M-Pesa.

Akidhibitisha kisa hicho siku ya Jumanne, OCPD wa Yatta Edward Kipsang alisema kuwa mshukiwa huyo alifumaniwa na umati wa watu wenye ghadhabu kabla ya polisi kumtia mbaroni.

Kipsang alisema kuwa mwanamume huyo amekuwa akisakwa na polisi kutokana na madai ya kuwaibia wahudumu wa M-pesa kwa muda mrefu.

"Mshukiwa huyo alifumaniwa na umati wa watu waliotaka kumwadhibu kabla ya polisi kumtia mbaroni,” alisema Kipsang.

Afisa huyo aliwaomba wahudumu wa M-pesa katika eneo hilo na wale waliokuwa wamepiga ripoti kuhusu wizi katika maduka yao kufika katika Kituo cha Polisi cha kithimani kubaini iwapo wanaweza kumtambua mshukiwa huyo.

Mshukiwa huyo sasa anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kithimani huku akisubiri kufikishwa mahakamani hapo kesho.