Share news tips with us here at Hivisasa

Polisi mjini Naivasha wanamsaka mfanyibiashara mmoja mashuhuri kuhusiana na wizi wa mbao za ujenzi zenye dhamani ya mamilioni ya pesa kwenye barabara kuu ya Nairobi kulekea Nakuru.

Kiwango fulani cha mbao hizo kinadaiwa kupatikana katika makaazi ya mfanyibiashara huyo eneo la Kayole huku lori lililokuwa likisafirisha bidhaa hiyo likipatikana katika mtaa jirani wa Kinamba.

Mkazi mmoja Paul Wang’ombe amesema kuwa gari lililokuwa na mbao hizo lilitekwa nyara.

Afisaa mmoja wa polisi na ambaye hakutaka kutajwa jina lake amedhibitisha tukio hilo na kusema kuwa wanamsaka mfanyibiashara huyo ili kurekodi taarifa.

“Tayari tuko katika harakati ya kumsaka mtu huyo na tutamfungulia mashtaka ikiwa atapatikana na hati,” alisema afisa huyo.