Share news tips with us here at Hivisasa

Maafisa wa polisi wa Waseges kwenye Kaunti ndogo ya Subukia, Kaunti ya Nakuru, wanamsaka jamaa mmoja anayedaiwa kumbaka msichana wa kidato cha nne kutoka Shule ya upili ya Tachasis.

Ripoti zinaarifu kuwa mwanafunzi huyo alikutana na jamaa huyo alipokuwa akielekea nyumbani kutoka shuleni, mwendo wa saa kumi na mbili unusu jioni.

Akizungumza na mwandishi huyu kwa njia ya simu siku ya Ijumaa, mwalimu mkuu wa shule hiyo Richard Lamulen, alisema kuwa mwanamume huyo alimsalimia mwanafunzi huyo na hapo akaanza kumfuata jamaa huyo kabla yake kuzirai.

Lamulen alisema kuwa hapo baadaye, msichana hyo alipatikana akiwa amezirai kwenye kichaka kimoja mjini Solai.

Aliongezea kuwa baada ya msichana huyo kupelekwa katika kituo cha matibabu cha Wei Wei, ilibainika kuwa alikuwa amebakwa.

Kwa muujibu wake, maafisa wa polisi walifaamishwa kuhusiana na kisa hicho na tayari wameazisha msako wa kumtafuta mshukiwa huyo.