Share news tips with us here at Hivisasa

Maafisa wa polisi mjini Nyamira wamehimizwa kuanzisha uchunguzi kuwatia mbaroni waalifu katikia mji huo na viunga vyake.

Ombi hilo limetolewa baada ya visa vya uhalifu kuongezeka kila uchao katika mji wa huo na viunga vyake ambapo duka la mkaazi mmoja lilifunjwa na kuibwa huku watu watatu wakiuawa kufikia katika eneo la Nyabite mjini Nyamira.

Wakizungumza siku ya Jumatano mjini Nyamira idadi kubwa ya wakaazi wa mji huo walisema wamehofia maisha yao na kuishi bila amani kufuatia uhalifu ambao hufanywa mjini humo.

“Hapa Nyamira tumeshindwa tutorokee wapi kwani hakuna usalama,' alisema Mose.

"tunaomba maafisa wa polisi kuanzisha uchunguzi kuwatia mbaroni wanaofanya uhalifu huo hapa Nyamira maana wengi wamepata hasara na wengine wamepoteza maisha yao,” aliongeza Mose.

Katika mji wa Nyamira na hata kaunti mzima hivi maajuzi visa vya uhalifu vimekuwa vikishuhudiwa kila mara huku polisi wakiomba kuimarisha usalama kila sehemu ya kaunti hiyo.

Ikumbukwe kuwa kamishina wa kaunti ya Nyamira Josephine Onunga alitangaza kuimarisha usalama zaidi katika kaunti hiyo jambo ambalo wakaazi wa kaunti hiyo wanadai halijatekelezwa kwani uhalifu unaendelea kutekelezwa.