Watu watatu wenye asili ya Kihabeshi wamenaswa katika eneo la Tonge Nyama Likoni wakiwa wamefungiwa ndani ya chumba.
Inaripotiwa kuwa mmiliki wa chumba alikuja na watu hao watatu asubuhi akawafungia ndani ya chumba na kuondoka.
Mwenye nyumba aliwafahamisha maafisa wa polisi ambao walikuja na kuvunja mlango na kuwanasa jamaa hao.
Mwandishi huyu alikuwepo wakati wa kisa hicho na inaarifiwa kuwa watatu hao hawaelewi lugha nyingine.
Watatu hao walikuwa na simu nyingi na walibebwa na gari la askari la kaunti.
Jamaa aliyekuwa amewahifadhi watu hao watatu alitoroka baada ya kuona maafisa wa polisi wamefika.
Polisi wameanza uchunguzi wa kumnasa jamaa aliyehusika kuwaficha watatu hao.