Naibu Rais William Ruto amepongezwa kwa kuitikia bewa la benki ya ‘Central Bank’ kuanzishwa mjini Kisii.
Hii ni baada ya naibu gavana wa kaunti ya Kisii Joash Maangi na viongozi wengine kuomba bewa la benki hiyo, kwani kaunti hiyo hutuma zaidi ya asilimia 65 ya fedha hadi benki hiyo mjini Nairobi.
Wakizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumatatu mjini Kisii, wakazi hao walimpongeza Ruto kwa yale aliyazungumza siku ya Jumapili ugani Gusii stadium kwa kuitikia tawi la benki hiyo kuazishwa mjini Kisii.
“Tumekuwa tukihitaji bewa la benki hiyo kuanzishwa hapa mjini Kisii na sasa tuko na furaha kwa sababu tunaenda kupata bewa hilo,” alisema Jeremiah Maobe, mkazi.
“Tunapongeza naibu rais kwa kuitikia bewa la benki hiyo kuletwa na hapa mjini Kisii na tunaomba mengi kufanywa kwetu kama wakazi wa Kisii,” aliongeza Maobe.
Aidha, wakazi hao waliomba serikali ya kitaifa kukarabati barabara ambazo serikali hiyo ilitoa ahadi ya kuzikatabati wakati walikuwa wanafanya kampeni na kuomba watimize ahadi hizo.
“Kile tunaomba sasa serikali ya kitaifa kutufanyia ni kutukarabatia barabara zile ilitoa ahadi ili sekta ya uchukuzi iwe shwari,” alisema Hesbon Nyakebako, mkazi mwingine.