Share news tips with us here at Hivisasa

Seneta wa Nairobi Mike Mbuvi ameutaka mrengo pinzani kumuheshimu kiongozi wa nchi iwapo una nia ya kuleta umoja kwa taifa hili.

Mbuvi alisema kwamba siasa za chuki anazoelekezewa kiongozi wa taifa huenda zikaligawanya taifa hili kikabila.

Akihutubia wananchi katika harambee ya kuchangia ujenzi wa bweni katika shule ya upili ya Mwanambeyu, Mbuvi alisema kwamba siasa za chuki zinazoendelezwa na baadhi ya wanasiasa huenda zikachangia uhasama baina ya jamii za nchi unaoweza kulitumbukiza taifa hili katika machafuko.

Aidha, aliwataka viongozi kujizatiti katika maswala ya maendeleo ya taifa na kuacha kulumbana kisiasa.

Kauli hii inajiri baada ya kushuhudiwa kuongezeka siasa za chuki na za lawama dhidi ya serikali ya mrengo wa Jubilee.

Tamko la Mbuvi lajiri huku joto la kisiasa likiwa limepanda kufuatia matamshi ya viongozi wa pande zote mbili, Cord na Jubilee, ambao wamekua wakirushiana cheche za maneno.