Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya Kaunti ya Kisii imeombwa kutoa kandarasi kwa vijana ili kuwawezesha kujiimarisha na kujiendeleza kimaisha.

Wito huo umetolewa baada ya kubainika kuwa idadi kubwa ya vijana katika kaunti hiyo wamesomea taaluma mbalimbali ambazo zinawawezesha kutekeleza miradi mbalimbali katika serikali ya kaunti, lakini hawajafanikiwa kupata kandarasi hizo.

Akizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumapili mjini Marani, mwanasiasa aliyewania kiti cha uwakilishi wadi katika wadi ya Sensi eneo bunge la Kitutu Chache Paul Angwenyi alisema vijana wengi wako na taaluma mbalimabli, lakini hawajapokezwa kandarasi zitakazi wasaidia kujikimu kimaisha.

“Tunaomba serikali ya kaunti yetu iwajali vijana wakati wa kupeana kandarasi. Vijana wetu wanapaswa kupokezwa kandarasi hizo ili wajiendeleze kimaisha,” alisema Angwenyi.

Wakati huo huo, Angwenyi aliomba serikali ya kaunti kuwapa ajira wakazi kutoka sehemu zote za kaunti ili kuonyesha uwazi na haki kwa wapiga kura.

“Tunaomba haki kutendeka kwa wakazi wote wa kaunti wakati wa kutoa ajira ili sehemu zote zinufaike na serikali za ugatuzi,” alisema Angwenyi.

Angwenyi aliomba kila mkazi wa kaunti ya Kisii kujaribu kupata kitambulishio na kadi ya kura ili kujitayarisha kuchagua viongozi watakaoleta maendeleo.