Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Serikali ya kaunti ya Kisii imedaiwa kubagua eneo bunge la Bomachoge Chache na Borabu katika miradi ya maendeleo.

Wakizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu katika eneo la Gucha wakaazi wa eneo bunge la Bomachoge wakiongozwa na David Abuya walidai kuwa serikali ya kaunti ya Kisii imewabagua katika miradi ya maendeleo jambo ambalo limewakera wakaazi hao.

Kulingana na wakaazi hao, kuna baadhi ya mashida yanayoikumba eneo hilo kama vile; kutokamilika kwa ukarabati wa barabara katika maeneo bunge hayo, kukosa vyoo katika masoko pamoja na kutoajiriwa kwa wakaazi hao katika serikali ya kaunti katika nyadhifa kuu serikalini.

Sasa wakaazi hao wameitaka serikali ya kaunti hiyo kuwajali na kuwafanyia miradi ya maendeleo kwani barabara nyingi hazipitiki haswa wakati huu mvua ya gharika inaendelea kunyesha katika sehemu mbalimbali nchini .

Hata hivyo wanahitaji kujengewa vyoo sokoni kwani wafanyibiashara hawana mahala pa kujisaidia wanapoendeleza shughuli zao za kibiashara .

“Sisi wakaazi wa Bomachoge tumeonekana kubaguliwa na serikali ya kaunti ya Kisii katika maendeleo, barabara nyingi za eneo hili hazipitiki tunashindwa pa kupita na tunaomba serikali itukarabatie barabarara,” alisema Abuya.

“Hakuna vyoo katika soko zetu,na hatujafanikiwa kupata kazi za ajira katika serikali ya kaunti ila tu ni wachache walipata kazi ya kufanya kazi  ya kuajiriwa kama askari wa kaunti huku maeneo bunge mengine yakikabidhiwa nyadhifa kuu za uwaziri, tunaomba serikali itujali kwa maendeleo,” alisema mkaazi Chris Osate.