Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali imeombwa kuweka matuta katika barabara kuu ya kutoka Kisii-Kebirigo ili kupunguza visa vya ajali vinavyoendelea kushuhudiwa kila mara.

Ombi hilo limetolewa baada ya mwendeshaji wa pikikpiki kugongwa kwa gari na kufariki papo hapo katika eneo la Konate katika barabara ya Kebirigo.

Kwa mujibu wa Joseph Onchiri waliomba serikali kuwapunguzia visa vya ajali katika barabrara hiyo kwa kuweka matuta kwani magari huendeshwa kwa kasi kufuatia ukosefu wa matuta .

“Tunaomba serikali kujali maisha ya binadamu kwa kuweka matuta katika barabara hii, kwani gari huendeshwa kwa kasi zaidi,” alisema Onchiri.

Aidha, walisema hii si mara ya kwanza visa vya ajali kushuhudiwa katika barabara hiyo na vinaendela kuongezeka kila uchao.