Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwenyekiti wa chama cha ODM eneo bunge la Matuga Hassan Chitembe, amedai kuwa Spika wa Bunge la kaunti ya Kwale Sammy Ruwa amechangia kuzorota kwa maendeleo katika kaunti hiyo.

Chitembe sasa anamtaka Ruwa kujiuzulu wadhfa wa Spika wa bunge la kaunti hiyo, akisema kuwa kunao viongozi wengine wengi wasomi wenye uwezo wa kuutekeleza wajibu huo.

Akiongea na wanahabari baada ya mkutano na viongozi wa chama cha ODM mjini Mombasa siku ya Ijumaa, Chitembe alihimiza kuwa na ushirikiano kati ya viongozi wa kaunti ya Kwale ili kufanikisha ajenda mbali mbali za kimaendeleo badala ya wao kuanza siasa za mapema.

“Tunamtaka Ruwa kujiuzulu kama spika wa bunge la kaunti ya Kwale iwapo yeye amejitolea waziwazi kuanza sasa za mapema na kujiunga na king’anga’anyiro cha kuwania ugavana wa kaunti ya Kwale ili apeyane nafasi kwa viongozi wengine kuwajibikia jukumu hilo,” alisema Chitembe.

Matamshi ya Chitembe yanajiri baada ya spika huyo wa bunge la kaunti ya Kwale kutangaza azma yake ya kuwania ugavana katika uchaguzi mkuu ujao.

Spika wa Bunge la kaunti ya Kwale Sammy katika mkutano wa hadhara wa kisiasa hapo awali. Alihimzwa kujihuzulu iwapo ana azmia kuwania ugavana wa kaunti ya Kwale na kujitosa katika siasa za mapema.