Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae amesema serikali yake itashirikiana na kampuni ya Kanuria kutoka nchi ya India kuhakikisha kilimo cha miwa kimeinuliwa kabla ya ujenzi wa kiwanda cha miwa kukamilika kujengwa.
Kulingana na Ongwae wakulima wa miwa wamekuwa wakikosa soko ambalo linawanufaisha kujiendeleza kimaisha kupitia kilimobiashara kwa muda mrefu.
Ongwae aliongeza kwa kusema kuwa wakulima hao watasaidiwa kujiinua kupitia miwa kabla ya ujenzi wa kiwanda hicho kukamilika, ujenzi huo unatazamiwa kukamilika mwaka wa 2018.
Akizungumza siku ya Alhamisi afisini mwake wakati wa kutia sahihi ya maelewano katika yeke na kampuni hiyo kutoka India, Ongwae alisema kilimo kimefanya wengi kujiendeleza na kuna haja wakulima kusaidiwa kujiendeleza.
“Kabla ya kiwanda cha miwa kukamilika kujengwa serikali yangu na kampuni ya kanuria ambayo itafanya ujenzi huo tutashirikiana kuhakikisha wakulima wa miwa wamesaidiwa kujiendeleza kimaisha kupitia kilimo cha miwa,” alisema Ongwae.
Kwa mujibu wa gavana Ongwae ujenzi wa kiwanda cha miwa utaanza rasmi mwezi wa sita mwaka huu na kukamilika mwaka wa 2018.