Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Spika wa bunge la Kaunti ya Nakuru Susan Kihika, ametoa wito kwa Wakenya kukumbatia umoja kwani ni nguzo muhimu katika kufanikisha maendeleo.

Kihika alisema ingawa ugatuzi unaidhinishwa nchini kuboresha maisha ya wananchi mashinani kupitia miradi tofauti, baadhi ya wanasiasa wanapotosha wananchi kwa kuwagawanya kwa mirengo ya kisiasa, kikabila na kidini.

Akiongea baada ya hafla ya mazishi ya Veronicah Wanjiku katika wadi ya Bahati siku ya Jumatano, spika huyo alisema taifa ambalo linataka kujikwamua kutoka umaskini lazima liwe na wananchi ambao ni wazalendo na wasiokubali kugawanywa.

“Wakati wa siasa haujafika kwa hivyo wanasisa wanapswa kuacha matamshi ya chuki ambayo huenda yakawagawanya wananchi. Wanapaswa pia kufahamu kuwa hakuna aliye juu ya sheria,” alisema Kihika.

Haya yanajiri huku siasa za uchaguzi wa mwaka wa 2017 zikianza kuchukua mwelekeo katika kaunti ya Nakuru.