Vijana mjini Nakuru wamekashifu vikali kufutwa kazi kwa aliyekuwa mkuu wa wafanyikazi Raymond Komen.
Komen alisema alipokea barua ya kufutwa kazi siku ya Jumatatu. Kufutwa kazi kwa Komen, ambaye ni kiongozi mwenye umaarufu huko Rongai, kumeibua msisimuko wa kisiasa.
Kwenye mtando wa Nakuru Analysts, vijana waliteta kuwa serikali ya kaunti ya Nakuru inazidiki kuwakandamiza vijana.
“Kufutwa kazi kwa Komen ambaye ni mmoja wa iongozi waliowakilisha vijana ni ishara tosha ya jinsi vijana hatambuliwe kwenye uongozi huu,” James Ekong alisema.
Aidha mjadala mkali uliibuka kuhusiana na swala hilo huku gavana Kinuthia Mbugua akikashifiwa vikali.
Komen alidai tofauti za kisiasa kati yake na gavana Kinuthia pamoja na naibu wake Joseph Ruto zilifanya afutwe kazi.