Shirika la kijamii la KICOSCE limeripoti kuwa hakuna uhusiano mwema kati ya askari na vijana eneo la Changamwe, jambo linalochangia vijana kujiunga na makundi ya kihalifu na hata yale ya kigaidi.
Shirika hilo limeeleza kwamba kuna haja ya askari kuondoa dhana ya kuwaona vijana ni wahalifu, na vijana kuondoa fikra ya kuwa askari ni maadui zao ili kuwe na ushirikiano mwema kati yao.
Vile vile shirika hilo limeripoti kuwa ukosefu wa kazi na viongozi kutothamini vijana inachangia vijana kujiunga na makundi ya uhalifu.
Ni kutokana na hilo ambapo mkuu wa polisi eneo la Changamwe Geoffrey Walumbe amewataka wananchi kuripoti kwa idara husika dhulma wanazopitia mikononi mwa polisi.
Aliyasema haya katika kongamano la vijana lilioandaliwa na shirika la kijamii la KICOSCE lililolenga kuhamasisha vijana kuwa na uhusiano mwema na polisi.