Zaidi ya vilabu 10 katika eneo la Mang’u kaunti ndogo ya Rongai zitafungwa kwa kutofwata sheria za uuzaji wa pombe.
Akizungumza katika eneo hilo Jumapili jioni, mwenyekiti wa NACADA John Mututho alisema kuwa, vilabu vingi eneo hilo viko karibu na shule jambo ambalo linaenedelea kuadhiri viwango vya elimu kwa wanafunzi wa eneo.
Aliongeza kuwa, vijana wengi kutoka Rongai na taifa nzima wanafariki kutokana na unywaji wa pombe haramu.
“Kila wakati tunawapoteza vijana wetu kutokana na pombe haramu na lazima hivi vilabu vifungwe vyote. Alisema Mututho.”
Alisema atahakikisha kuwa, vilabu hivyo vimefungwa na wamiliki kuchukiliwa hatua Kali za kisheria.
Swala hili limejiri Siku chache tu baada ya vijana wawili kufariki kwa kuhusika kwenye ajali katika eneo hilo la Mang’u wakiwa walevi.